Lai Marketing Agency

hello@laimarketing.co.tz

JINSI WASANII WANAVYOWEZA KUTUMIA MITANDAO YA KIJAMII KUTANGAZA NYIMBO ZAO MPYA

Mitandao ya kijamii licha ya kuwa sehemu nzuri kwa wafanyabiashara kutangaza, kuuza na kununua bidhaa na huduma  lakini pia imekuwa  sehemu kubwa kwa wasanii wa muziki kuwafikia walengwa wa kazi zao kwa urahisi na haraka zaidi.

Siku hizi watu wengi wamekuwa wakitumia muda mwingi na simu zao hasa kwenye mitandao ya kijamii, jambo ambalo msanii lazima utengeneze mkakati wa namna ya kutumia mitandao ya kijamii ili kuwafikia walengwa wako

Kwa upande wa Tanzania kuna wasanii wamekuwa wakiweka nguvu kubwa kwenye mitandao ya kijamii yawezekana hata kuliko njia zozote  kila wanapotoa nyimbo zao. Hii imeondoa dhana ya kutegemea njia moja tu kama redio , Tv au magazeti kutangaza nyimbo zao .

Leo tutaangalia njia tano muhimu ambazo zimekuwa zikitumiwa na wasanii wakubwa na wadodo kila wanapotoa nyimbo zao katika kutumia  mitandao ya kijamiii kuwafikia walengwa wao kiharaka na urahisi zaidi.

1: TENGENEZA MPANGO KAZI (STRATEGY)

Mitandao ya kijamii inampa uhuru mtumiaji kusikiliza na kuangalia kile anachokitaka tofauti na njia nyingine. Ukiwa huna mkakati mzuri basi ni ngumu walengwa wako kuwapata wote kupitia mitandao ya kijamii.

Anza kutengeneza brand yako (Chapa) kwa kuwa na picha moja kwenye mitandao yote ya kijamii ili kuwafanya watumiaji wakutambue kirahisi. Kama unatumia Ukurasa (Page) kwenye facebook , basi pale kwenye  Facebook cover weka video badala ya kuweka picha kama ilivyozoeleka . Pia unaweza kumtafuta mpigaji  picha mzuri ambaye unaweza kuwa unamlipa ghrama nafuu kati ya 1000 -2000/= kwa picha moja . Hakikisha kila picha inayoenda mtandaoni basi inasimamia maudhui yako na  uvaaji wako wa kitofauti zaidi.

2: ANDAA MAUDHUI YA KUWEKA MTANDAONI

Mpango kazi wako wa kutumia mitandao ya kijamii unatakiwa ugawanywe kupitia maudhui uliyoyapangilia kuyawakilisha. Hakikisha kunakuwa na mudhui yanayofanana kwenye kila mtandao wa kijamii ingawa unaweza ukatengeneza mpango kazi wa uwasilishaji wa maudhui kwa kila mtandao wa kijamii ili mradi usitoke nje ya lengo . Hii ina maana kuwa kila mtandao una watu wake tofauti  mfano watumiaji wa Twitter wanaweza kuwa tofauti na wale wa facebook au Instagram au Linkedin.

Anza kwa kuandaa stori zako mbalimbali, watu wanapenda sana stori na kufuatilia jinsi msanii anavyoishi nah ii ndo maana REALITY SHOW zote za Tv zimekuwa zikipendwa sana. Unaweza kuandaa stori ulivyoanza ,mafanikio,  changamoto, matamasha uliyohudhuria na pengine ukaweka Behind the scene .

Weka maudhui ya kuelimisha wafuasi wako, wafuasi wako wanapenda kujua kitu gani kingine unacho ukiachana na mziki unaweza kuwafundisha . Je wewe labda ni mchezaji mzuri wa mziki au wewe ni muandishi mzuri wa mashairi ukawafundisha wafuasi wako.

Weka maudhui ya kuwafurahisha wafuasi wako, kama unahisi una kitu cha kuwafurahisha mashabiki wako basi tumia jukwaa hilo kuwafurahisha wafuasi wako. Hakiksha lakini hautoki nje ya lengo au dhamira kuu

Weka maudhui yako ya msiamamo wako , kila msanii anakuwa na kitu anachokiamini kama mpira, siasa, biashara au mziki wenyewe . Kwa hapa kile unachokiamini lazima kiwe kinaendana na maudhui yako ya awali. Wasanii wengine wanachukua msimamo ambao unapendwa na wengi na hivyo mwisho kujizolea mashabiki wa upande huo.

3: MUUNDO WA MAUDHUI YAKO

Hakiksha muundo wa maudhui yako unakuwa kwenye mfumo ambao hauondoi  wazo kuu la awali ili kuwafanya wafuasi wako wakuelewe kwenye maudhui flani.

Kuna Maudhui ya video ,kuwa na maudhui yaliyopangiliwa ili kuwafanya watu waangalie mpaka mwisho video uliyoiweka kwenye  mitandao ya kijamii. Mara nyingi video nzuri inatokana na mpangilio mzuri wa matukio yanayoonyesha mwanzo, katikati na mwisho.

Maudhui ya Maneno;  Baada ya kujua lengo lako na msimamo wako ni rahisi kuanza kuandika maneno kwenye mitandao mbalimbali yenye kuruhusu maneno mengi kama MEDIUM na LINKEDIN ili kuwafanya wafuasi wako waendelee kukusoma na kukufahamu zaidi.

Maudhui ya picha : Maudhui ya picha mara nyingi hayawezagi kusimama yenyewe bila maneno, hakikisha unaweka maudhui kwa chini kwenye kila picha. Kama watu watachangia maoni au furaha yao basi lazima uhakikishe na wewe unawajibu.

4: PELEKA MAUDHUI YAKO KWENYE MITANDAO YA KIJAMII

Baada ya kuandaa maudhui , Hakikisha unawaelewa wafuasi wako vizuri kwa kila mtandao wa kijamii. Kila mtandao wa kijamii una faida na hasara. Maudhui yako ya facebook yanweza kuwa tofauti na maudhui ya instagraam baada ya kuwasoma vizuri wafuasi wako. Lakini kwa sehemu kubwa nchini Tanzania bado wasanii wengi hasa wadogo hawajui au hawapo kwenye mitandao mingi ya kijamii kama Twitter na  Linkedin  kupoteza mashabiki wa kazi zao.

5: SAMBAZA MAUDHUI YAKO SASA

Baada ya kuweka kwenye maudhui yako , usije ukabweteka na kusema kazi imeisha.Anza kwa kusambaza maudhui yako ili yaweze kuwafikia wengi.

Andaa Hashtag (#) ambayo itawaunganisaha mashabiki na wafuasi wako kupitia mitandao mmoja au yote ya kijamii. Andaa hashtag isiyotoka nje ya maudhui yako ya awali au jina la nyimbo yako, waambie mashabiki wako watumie hiyo hashtag kutoa maoni, au ujumbe wowote kwako. Kuna Application mbalimbali za kulipia na za bure katika kupata maoni ya wafuasi wako wote mtandaoni.

Andaa timu ya watu wenye wafuasi wengi mtandaoni ambao watakusaidia kutangaza nyimbo yako, hapa unaweza kuwaomba na kuwalipa hela kidogo kwa kutegemeana na mtandao unaotumia . Ni njia iliyozoeleka sana na inatumiwa na wasaniii wengi . Hakikisha wanatumia hashtag ilimwisho uweze kujua ni wangapi wameona kazi yangu na nimewafikia kwa sehemu gani.

Tengeneza ushindani wa kimaudhui kati yako na msanii mkubwa na omba wafuasi wako watoe maoni, mfano unaweza kuchukua kipande cha mstari alichoimba msanii flani na ukaweka kipande chako kinachofanana kimaudhui na ukawaomba wafuasi wako watoe maoni.

Kuna Njia ya Dancer au kikundi cha vijana  wakicheza  nyimbo yako, hapa unaweza kuandaa ni kikundi gani kimecheza vizuri zaidi na ukawaomba mashabiki wachague mshindi na ukawapa zawadi ndogo . Njia nyingine ni  watoto wakiimba nyimbo yako katika staili yenye ubunifu mkubwa wa nyimbo yako.

Kujitolea kwenye miradi ya kijamii , hii pia inafanya washabiki waone kama ni mtu ambao upo karibu yao na hivyo kuwa karibu na kile unachokifanya . Picha zote unazopiga na wanajamii hakiksha ziko katika kiwango kile kile cha juu au kinachofanana toka mwanzo.

Matangazo ya kulipia kupitia kwenye mitandao ya kijamii, kwa upande wa Facebook na Instagram wanakukopesha dola za kimarekani  $25 kwa kila aliyekamilisha usajili wote kwenye mitandao hii. Hela hii utaitumia kulipia matangazo ambayo unataka kuwafikia watu wengi zaidi kwenye mitandao ya kijamii. Hapa pia hakiksha kuna lengo kuu la kukufanya ulipie hii huduma, na ikumbukwe facebook wanaitaka fedha hii mwishoni mwa mwezi  bila ya riba.

Wasanii wengine wadogo walioko mikoani wamekuwa wakitumia kitu ambacho kinasifika zaidi kwenye mkoa wake na kujiambatanisha nacho ambapo inakuwa rahisi watu kukujua haraka na kupata wafuasi wengi kwenye mitandao ya kijamii.

Share on facebook
Facebook
Share on twitter
Twitter
Share on linkedin
LinkedIn

4 thoughts on “JINSI WASANII WANAVYOWEZA KUTUMIA MITANDAO YA KIJAMII KUTANGAZA NYIMBO ZAO MPYA”

  1. Excellent article. Keep posting such kind of info on your blog.
    Im really impressed by your site.
    Hello there, You’ve performed an incredible job. I’ll certainly digg it
    and for my part recommend to my friends. I am sure they will be benefited from this
    web site.

  2. Your style is really unique in comparison to other people I
    have read stuff from. Thank you for posting when you have the opportunity, Guess I will just book mark this blog.

  3. Just want to say your article is as astonishing.
    The clarity in your post is simply excellent and i can assume
    you’re an expert on this subject. Well with your permission allow
    me to grab your feed to keep up to date with forthcoming post.
    Thanks a million and please continue the enjoyable work.

  4. Simply want to say your article is as amazing.
    The clarity in your post is just excellent and i could assume you are an expert on this subject.
    Well with your permission let me to grab your RSS feed to keep up to date with forthcoming post.
    Thanks a million and please continue the rewarding work.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Have Any Question?

Lai agency is a full-service marketing and media agency specializing in digital branding, experiential marketing, videography, photography, digital marketing, web developments, training, and Search Engine Optimizations (SEO).